Monday Apr 03, 2023

Injili ni Jibu

Unasikiliza ShareLifeAfrica!

Jinsi tunavyofikiri kuhusu Injili huathiri moja kwa moja ikiwa tunashiriki au la. Je, tunaiona kweli kuwa Habari Njema? Injili ina maana gani kwetu?

Yesu aliporudi Nazareti wakati wa huduma Yake, alitembelea sinagogi, ambako Alisoma kitabu cha kukunjwa cha Isaya. Ndipo Yesu akatimiza unabii uleule aliosoma: “Roho wa Bwana yu juu yangu, kwa maana amenitia mafuta kuwahubiri maskini Habari Njema. Amenituma kuwatangazia wafungwa uhuru wao, na vipofu kupata kuona tena, kuwaacha huru waliosetwa.”

Tunapokubali kwamba Injili ndiyo njia ya kuponya ardhi yetu, kuleta uhuru kwa wafungwa, na kutoa hazina isiyo na kifani kwa maskini, matendo yetu yanabadilika sana. Kwa hivyo basi hebu tulete Habari Njema hii kwa maskini, wagonjwa, na ulimwengu unaoumia unaotuzunguka. Injili ndio jibu. Na ni Habari Njema kwa wote wanaoisikia!

Jifunze jinsi unavyoweza kuwa sehemu ya kushiriki Injili kwa kutembelea tovuti yetu katika sharelifeafrica.org

Comments (0)

To leave or reply to comments, please download free Podbean or

No Comments

Copyright 2022 Evangelism Explosion International - Africa Ministry. All rights reserved. https://www.sharelifeafrica.org

Podcast Powered By Podbean

Version: 20241125