
Monday Aug 21, 2023
Omba Kuokoa
Unasikiliza ShareLifeAfrica! Je! ni nani unayetaka kumjua Yesu? Je, una jina? Je, unamwombea mtu huyo? Je, umepata mwamini mwingine wa kuwaombea pamoja nawe?
Miaka michache iliyopita, mchungaji wa vijana katika kanisa langu alikusudia kuwafunza vijana ili kuwaombea marafiki zao waliopotea. Huduma ilianza kuombea zaidi ya watu mia moja na arobaini (140); na katika miezi miwili tu ya kwanza, kumi na wanane kati ya marafiki hao walikuja kwenye imani yenye kuokoa katika Yesu! Hiyo ndiyo nguvu ya kuwaombea waliopotea pamoja! Je, unaweza kufikiria nini kingetokea katika maisha ya waliopotea unaowapenda ikiwa ungekusanyika pamoja na waumini wengine kuwaombea?
Moyo unaoomba pia ni moyo uliofunguliwa kwa kushiriki Injili, vivyo hivyo fanya vile Bwana anavyokuongoza na uangalie anapohamisha milima kuwaokoa waliopotea na wanaoumizwa. Kwa nyenzo za kukufanya uanze kushiriki imani yako, tembelea tovuti yetu katika sehemu ya maisha leo, kwa vidokezo, zana na nyenzo za kukusaidia: ShareLifeAfrica.org
Comments (0)
To leave or reply to comments, please download free Podbean or
No Comments
To leave or reply to comments,
please download free Podbean App.