Tuesday Jan 14, 2025

Saa Imekaribia

Katika Warumi kumi na tatu kumi na moja (13:11), Paulo anatuambia, “Fanyeni hivi, mkiujua wakati, kwamba saa ya kuamka katika usingizi imekwisha kuwadia; kwa maana sasa wokovu u karibu nasi kuliko tulipoamini.” 

Vema, anamaanisha nini anaposema, “fanya hivi?” Ili kujua hilo, inatubidi kurejea mistari michache ambapo Paulo anawasihi Wakristo wa kanisa kupendana na kuwapenda jirani zao. Anawaita kwenye uaminifu na kuwatumikia waamini wenzao na jumuiya zao. Kwa kweli, tunajikuta katika siku ambazo kujitolea kwa Mungu katika kiwango hicho kunaweza kutugharimu kitu. 

Lakini ninataka kukutia moyo leo—inafaa. Unapochagua kuwapenda wengine kwa kushiriki Injili nao, unaona maisha zaidi yakibadilishwa kwa utukufu wa Mungu. Na siku ile Kristo atakaporudi inakuja haraka kuliko tunavyofikiri. Kwa hiyo tuwe waaminifu kushiriki upendo wa Mungu na wengine.

___________________________________

ShareLifeAfrica ni redio ya Kikristo na kipindi cha podikasti cha Evangelism Explosion International Africa Ministry; ambayo imejitolea kukupa zana na nyenzo zinazohitajika ili kushiriki imani yako na wengine kwa ujasiri na kwa ufanisi.

Comments (0)

To leave or reply to comments, please download free Podbean or

No Comments

Copyright 2022 Evangelism Explosion International - Africa Ministry. All rights reserved. https://www.sharelifeafrica.org

Podcast Powered By Podbean

Version: 20241125