Monday Jan 22, 2024

Wakati wa Neema ya Mungu

(Msimu wa 48: Kipindi cha 01)

Paulo ananukuu katika Wakorintho wa pili sita mbili (6:2) maneno haya kutoka kwa Isaya, “Wakati wa upendeleo wangu nalikusikia, na siku ya wokovu nalikusaidia.” Paulo anaendelea kwa kusema, “Nawaambia, sasa ndiyo wakati wa neema ya Mungu, sasa ndiyo siku ya wokovu.”

Na ningesema vivyo hivyo kwako leo! Hatujui wakati tulio nao. Hatujaahidiwa kesho. Kwa hiyo leo ndiyo siku ya kushiriki habari njema zaidi ambayo mtu mwingine anaweza kusikia—na huo ni wokovu kupitia Yesu. Ikiwa unafikiria juu ya maisha yako mwenyewe, kulikuwa na siku, saa, sekunde ambayo unaweza kuwa umefanya uamuzi huo mwenyewe, na Yesu akawa Mwokozi na Bwana wako.

Leo inaweza kuwa siku hiyo kwa mwingine. Roho Mtakatifu ni mwaminifu kubadili mioyo. Tunapata fursa ya kuwa sehemu ya mchakato kwa kushiriki Injili. Kwa nyenzo za kukusaidia kushiriki imani yako, tembelea sharelifeafrica.org
___________________________________

ShareLifeAfrica ni redio ya Kikristo na kipindi cha podikasti cha Evangelism Explosion International Africa Ministry; ambayo imejitolea kukupa zana na nyenzo zinazohitajika ili kushiriki imani yako na wengine kwa ujasiri na kwa ufanisi.”

Comments (0)

To leave or reply to comments, please download free Podbean or

No Comments

Copyright 2022 Evangelism Explosion International - Africa Ministry. All rights reserved. https://www.sharelifeafrica.org

Podcast Powered By Podbean

Version: 20241125