Thursday Feb 15, 2024

Yesu Kristo

(Msimu wa 51: Kipindi cha 04)

Leo tutajifunza uwasilishaji wa Injili ulio rahisi kukumbuka. Mpangilio wetu wa kushiriki Injili unategemea maneno makuu matano - Neema, Mwanadamu, Mungu, Kristo, na Imani na tunaunganisha kila mmoja kwa kidole cha mkono wetu kama msaada wa kujifunza.

Leo tutazingatia neno la nne - piga picha kidole chako cha pete na umfikirie Bwana Arusi kwa sababu neno la leo ni KRISTO. Yesu Kristo ni Mungu na Mwanadamu. Injili ya Yohana inaanza kwa msisitizo huu, “Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu…Naye Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu.”

Ingawa Yesu alikuwa na mafanikio mengi makubwa, hakuna shaka kuhusu Yake muhimu zaidi:  Alikufa msalabani ili kulipa adhabu ya dhambi zetu…na akafufuka kutoka kwa wafu ili kuthibitisha kwamba Ametununulia mahali Mbinguni. Zawadi hii inapokelewa kwa imani. Unaweza kutembelea ShareLifeAfrica.Org kutazama video inayoonyesha Uwasilishaji wa Injili kwa Mkono. Hiyo ni ShareLifeAfrica

___________________________________

ShareLifeAfrica ni redio ya Kikristo na kipindi cha podikasti cha Evangelism Explosion International Africa Ministry; ambayo imejitolea kukupa zana na nyenzo zinazohitajika ili kushiriki imani yako na wengine kwa ujasiri na kwa ufanisi.”

Comments (0)

To leave or reply to comments, please download free Podbean or

No Comments

Copyright 2022 Evangelism Explosion International - Africa Ministry. All rights reserved. https://www.sharelifeafrica.org

Podcast Powered By Podbean

Version: 20241125