
Monday May 29, 2023
Yesu ni kimbilio letu
Unasikiliza ShareLifeAfrica! "Mungu kwetu sisi ni kimbilio na nguvu, Msaada utakaoonekana tele wakati wa mateso. Kwa hiyo hatutaogopa..."
Mistari hii yenye nguvu kutoka kwa Zaburi ya arobaini na sita inatukumbusha ukweli muhimu unaopatikana katika Neno la Mungu—tunapofanyika watoto wa Mungu, Yesu ndiye kimbilio letu. Kwa hakika, jambo la mwisho ambalo Yesu aliwaambia wanafunzi wake kabla ya kupaa mbinguni lilikuwa, “...hakika mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari. Huenda kuna mambo mengi tunayoogopa au kupigana nayo. Lakini leo, nataka kukuhimiza: Tafuta kimbilio lako kwa Yesu. Atakuwa Mwamba wako, Ngome yako, Ngao yako dhoruba zitakapokujia. Unaweza kutulia ndani Yake. Na kujua ukweli huu muhimu hubadilisha kila kitu. Inatupa nguvu ya kufanya yale ambayo Yesu aliwaambia wanafunzi wake wafanye kabla hajawaambia kwamba atakuwa pamoja nao daima: “Kwa hiyo enendeni mkafanye wanafunzi kutoka kwa mataifa yote.
Kwa zaidi kuhusu jinsi unavyoweza kutimiza Agizo Kuu kwa kushiriki imani yako, tembelea tovuti yetu katika sharelifeafrica.org
Comments (0)
To leave or reply to comments, please download free Podbean or
No Comments
To leave or reply to comments,
please download free Podbean App.